JIPATIE BLOG YAKUKULIPA 2020~Part 1


JINSI YA KUDESIGN BLOG INAYOLIPA
------------------PART 1---------------------
Habari wadau wangu wa nguvu wa blog yangu ya Sirlemsontechnologies.blogspot.com
Awali ya yote ijulikane wazi mimi binafsi sina blog inayolipa bali nitakufundisha yale ambayo nimepata kuyasoma na kuayaelewa ili kuwa na blog inayolipa.
NB: Na wakati huo huo nitoe angalizo kwamba usiache kazi yako ya kuajiriwa au kazi nyingine uliyojiajiri na ukahamia kublog ukitegemea utapata hela za kukutosha kuendelea na maisha yako! Ni kweli unaweza kupata pesa kwa kuwa na blog lakini ni jambo linalohitaji muda, miezi kadhaa na hata miaka wakati mwingine mpaka uje uone hela ikitoka kwenye hiyo blog na kuja kwako.
BLOG ni nini?
Neno Blog linatokana na maneno mawili ya kiingereza ambayo ni-;
web logs',. Neno Logs' tafsiri yake ni  kuweka kwenye rekodi'.
Hivyo Blog ni aina ya tovuti au website ambayo inaongezwa makala mpya kila mara kwa mpangilio maalumu. Kuna aina kuu 2 za blog, blog za bure na bure za kulipia.
Kwenye makala hii tutajadili zaidi kuhusiana na blog za kulipia sababu ndizo zinazoweza kulipa.
Ili kudesign blog inayolipa unahitaji vitu hivi kwa kuanzia;
1. Top Level Domain (T.L.D)
Domain ni nini?
Domain ni JINA LA BLOG. Hivyo jamiiforums.com au millardayo.com/ yote haya ni majina ya blog au tovuti.
Domain au jina la blog huwa na sehemu kuu mbili, mzizi (jina) na kiambishi tamati (extension)
Hivyo jamiiforums na millardayo haya yote mawili ni sehemu ya mzizi wa jina
na .com ndiyo kiambishi tamati au domain extension kama tulivyozoea
Sasa, top level domain ni domain za namna gani?
Ili uwe na blog inayolipa kitu cha kwanza ni kuwa na top level domain, hizi domain ambazo kwanza hazipatikani bure, ili kuwa nayo ni lazima ununue na mara nyingi unaweza kununua na kuimiliki kwa mwaka mmoja au miwili au hata zaidi kadri utakavyolipia wewe.
Pili, hizi top level domain mara nyingi ni kuwa, mara tu baada ya jina basi kinachofuatia ni kiambishi tamati (extension), mfano jamiiforums baada tu ya jina mwisho ni .com hivyo unasoma jamiiforums.com
Kumbe zile ambazo siyo top level domain kwanza ni bure na unakuwa huna umiliki wake kwa asilimia 100, hivyo unaweza ukaamka tu siku moja na usiione blog yako hewani na ukiuliza utaambiwa inakiuka vigezo na masharti yetu, hata kama si kweli!
Siyo hivyo tu, zile ambazo siyo top level domain huwa pia ni ndefu zaidi kuliko hizi top level domain kwa sababu katika hilo hilo jina lako kutatakiwa kuwepo pia jina la aliyekupa hiyo domain bure au wakati mwingine unaweza ukalazimishwa kiambishi tamati (extension) kiweje.
Hivyo ukitaka kuwa na blog inayolipa sahau kuhusu .blogspot.com, .wordpress.com, .webly.com na mengine mengi kama hayo.
Tuchukulie mfano kama hawa jamiiforums wangeamua kutumia jina la bure kutoka google kwa mfano, jina lao lingekuwa linasomeka hivi => jamiiforums.blogspot.com !!!
Umeona tofauti ya jamiiforums.com na
jamiiforums.blogspot.com?
Hivyo top level domain kwanza ni fupi na hivyo linakuwa rahisi hata kutamkwa na kukumbukika kirahisi. Ni rahisi kutaja au kutamka jamiiforums.com kuliko kutaja au kutamka na kukumbuka jamiiforums.blogspot.com
Watu wengi wanaotaka kuwa waandishi wa kujitegemea kwenye mtandao (bloggers) wengi hukosea kwa kutumia muda mrefu wakiwa na domain au majina ya blog ya bure. Haidhuru kutumia jina la bure lakini iwe ni kwa ajili ya kujifunza na kupata uzoefu tu kwa muda mchache, baada ya muda au hata mwanzoni kabisa kama unataka kuwa na blog inayolipa ni vema kuwa na top level domain mapema. Siyo gharama, top level domain unaweza kuipata kuanzia Tsh 10000 na haizidi Tsh 30000 labda iwe ni special sana kama zilivyo za .academy
VITU VYA KUZINGATIA UNAPONUNUA DOMAIN
Domain au jina zuri la blog lazima liwe na sifa zifuatazo;
1. Liwe Fupi, kwanini liwe fupi? ili iwe rahisi kutamkwa na kukumbukwa
2. Liendane na maudhui ya blog. Mfano unaona jamiiforums limebeba maudhui au malengo ya blog, jamii ni sisi watumiaji wote na forums ndivyo yalivyo majukwaa. Hii si kanuni hasa kwa blog binafsi zile mtu anaweza kuamua kutumia jina lake kamili na ndani yake akaandika lolote analolipenda au kuhusiana na taaluma au kazi yake.
Mara nyingi nikipata mtu anataka nimshauri kuhusu blog yake afanye nini iende mbele, cha kwanza nawaambia nitajie blog yako, nikiona tu ni jina la bure basi cha kwanza hata kabla sijaitembelea hiyo blog nitakuambia nunua jina.
Hatua ya kwanza katika kuwa na blog inayolipa ni kuwa na blog yenye jina la kulipia na siyo la bure. Na sababu ni nyingi, kwanza linakuwa ni la kwako kwa asilimia 100, unaweza kulifupisha kadri uwezavyo na linakufanya uonekane upo makini na kazi yako.
Kwa leo tuishie hapa, somo litaendelea na sehemu ya pili.
NB: Kwa wewe unaehitaji kupata Blog inayolipa njoo 📩 0762647448-Sir Lemson au tia comment hapa 👇👇 ili tuende pamona...
Kikubwa umeelewa kunaza free domain na paid domain
Hvyo utachagua mwenyewe
Bei zangu ni sawa na bure tuu
           KARIBU SANA
BY SIR LEMSON TECHNOLOGIES