JINSI YA KUDESIGN BLOG INAYOLIPA Part 4(Mwisho)

                          
JINSI YA KU-DESIGN BLOG INAYOLIPA

------------------PART 4------------------
2. Huwezi kuwa na blog yenye uzito (gb) wowote utakao wewe kwa mfano unaweza kuambiwa blog au website yako isizidi ukubwa wa mb 300 (disc space).
3. Unaweza pia ukaambiwa unaweza kuwa na barua pepe/email 1 au 2 au ukaambiwa huwezi kuwa na barua pepe kwa jina la blog yako mfano ukihifadhi blog yako kwenye google basi email yako haiwezi kuwa info@fadhilipaulo.com badala yake utalazimika kutumia email ya gmail! <= sasa kama upo makini na kazi yako huwezi kukubali vitu kama hivi.
Lakini yote hayo ni kwa sababu ya bure.
4. Ukiwa kwenye server ya bure wakati mwingine huwezi kujipangia ni mfumo upi utaumia kusanifu (to design) blog yako mfano kama upo kwenye server za google (blogspot) muundo au design ya blog yako lazima iwe ni zile za blogger tu, huwezi kuwa kwenye blogspot halafu utumie muundo (design) au mfumo wa blog unaotumia wordpress. Kadharika ukiwa .wordpress huwezi kutumia muundo wa blog wa blogger, drupal, joomla na kadharika.
Kumbe ukiwa kwenye server ya kulipia unaweza kuamua mwenyewe blog au website yako iendeshwe kwa mfumo upi ikiwa ni code (html) au utumie mfumo mwingine wowote wa kuendeshea blog (CMS), kama ni wordpress, blogger, html, drupal, Joomla na kadharika na kadharika kadri utakavyo wewe.
Kitu kingine kitakachokugharimu ukiamua kutumia server za bure ni vile namna ya kuifanya blog yako ionekane kirahisi kwenye injini za kutafutia vitu kwenye mtandao kama vile google, bing, nk. Hili tunaliita Search Engine Optimization (S.E.O), kumbe ukiwa kwenye server ya kulipia unakuwa na namna nyingi ya kulifanikisha hili kirahisi zaidi.
Kwa kifupi ukiwa na server yako ya kulipia kila kitu ni chako, haijalishi muundaji wa website kama ni kampuni au mtu binafsi, unao uwezo wa kufanya lolote kuanzia backups and restoration, kubadili mfumo wa blog wakati wowote na bila kumwambia yeyote.
Binafsi nilitumia server za bure mwanzoni mwa safari hii yangu ya kublog lakini baadaaye niliachana na hizo na nikaanza kulipia baada ya kuona kuna vitu vingi navikosa, kisha idadi ya wasomaji wangu waliendelea kuongezeka hivyo isingewezekana tena kukaa kwenye server za bure au server ndogo ndogo za kulipia.
Kuna server za kulipia za aina nyingi, lakini kabla ya kuamua ununuwe au ulipie ipi inakupasa kwanza kujuwa mahitaji yako na umhimu wa hiyo blog kwako na kwa wasomaji wako. Katika yote, nakushauri ulipie server inayokufanya uwe na &#8216;Personal Control Panel'. Control Panel (CPanel) ni aina ya mfumo wa kuhifadhia (host/serve) blog au website kwa namna ya pekee, na unapewa vitu vingi vinavyobaki kuwa vyako na unaweza kuiendesha blog au website yako kwa namna au mfumo wowote uutakao.
Labda utakuwa unajiuliza sasa ni bei gani kuwa na stoo/server yako ambayo ni ya kulipia na siyo ya bure? Jibu ni kama lilivyo kwa domain. Ni bei rahisi sana ingawa bei itaongezeka taratibu kadri blog yako inavyokuwa, kwa sehemu kubwa unaweza ukalipia kuanzia 5000 mpaka laki kadhaa au milioni kadhaa kwa mwezi kutegemea na ukubwa wa hiyo blog na ukubwa hapa huwa ni idadi ya watembeleaji na ukubwa wa faili la blog yako ambalo huongezeka ukubwa kadri unavyoandika makala mpya.

Karibu sehemu ya nne naya mwisho